Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, amesema baadhi ya watu wamejimilikisha ajenda ya mabadiliko, akisisitiza kuwa chama hicho hakiwezi kuwa mfuasi wa ajenda za kisiasa zinazoanzishwa na vyama vingine.
Jussa ameyasema hayo leo, Agosti 12, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana, ambapo amesema ACT-Wazalendo kimejijenga kwa misingi na misimamo yake ambayo imekuwa ikifahamika kwa wananchi.
Amesema chama hicho kitaendelea kusimamia ajenda zake kwa kujiamini badala ya kuwa “mkia” wa vyama vingine kwa kufuata misimamo au agenda zinazoanzishwa na wengine.
“Chama chetu kimenyooka sawa sawa na ajenda zetu zinafahamika,” amesema Jussa.
Amesisitiza kuwa ACT-Wazalendo itaendelea kushikilia misingi yake na kusimamia masuala inayoyaamini, huku ikiwataka wanachama na wafuasi wake kuendelea kuwa na msimamo katika kutekeleza ajenda za chama.




