Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 8, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka Mhe. Paul Christian Makonda (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Makonda alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo.




