Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ado Shaibu Ado ametembelea Ofisi za Makao Makuu za Chama cha Watu Wenye Ualibino Tanzania (TAS) na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama hicho juu kujenga ushirikiano wa kushughulikia haki na ustawi wa watu wenye ualbino Wilayani Tunduru.
Kwa upande wao TAS wamempongeza kiongozi huyo kwa kuwatembelea na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Ofisi ya Mbunge na Serikali ya Wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kuboresha ustawi wa watu wenye ualbino Wilayani Tunduru.
Naye Ado Shaibu ameahidi kushirikiana na TAS na Asasi nyingine kwenye jamii zinazosimamia haki za watu wenye ulemavu katika kujenga msingi katika kushughulikia changamoto za watu wenye ulemavu katika Jimbo la Tunduru Kaskazini.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 7 Januari 2026 katika Ofisi za Makao Makuu za TAS zilizopoa Dar es salaam.




