Saturday, March 21, 2026
spot_img
HomeHabariMstaafu awatahadharisha wenzake dhidi ya utapeli

Mstaafu awatahadharisha wenzake dhidi ya utapeli

Dinnah Ngowo, mstaafu anayepokea Pensheni Mfuko wa PSSSF,  amewatahadharisha wastaafu kuwa makini na watu wanaowapigia simu na kuwapa maelezo yanayohusiana na malipo ya pensheni zao.

“ Wastaafu wenzangu, hivi sasa wapi watu mtandaoni wanaozungumza mambo ambayo si ya kweli, ukipata taarifa yoyote kabla ya kufanya uamuzi fika kwenye ofisi husika.” alisema.

Ngowo ametoa tahadhari hiyo baada ya kufanikiwa kuukwepa ‘mtego’ aliowekewa na matapeli wakimuelekeza kufuatilia malipo ya nyongeza ya pensheni, ilihali hakukuwepo madai yoyote.

“Walinipigia simu kuwa nilitafutwa kwa simu na watu wa Hazina lakini sikupatikana, niko katika kundi la wastaafu walioongezwa pensheni na akanitajia kiwango, hivyo faili limewekwa kando halikushughulikiwa.” alisema.

Alisema, kimsingi mimi sipokei pensheni kutoka Hazina, lakini nikaenda huko Hazina walikonielekeza, lakini nilipofika; nikaelezwa hakuna kitu kama hicho. Nilipompigia aliyenipa taarifa hiyo kuwa nimekwenda Hazina na nimeambiwa hakuna taarifa hizo, nilichoambulia ni matusi mazito.” alifafanua.

Hata hivyo, alipofika PSSSF kutoa taarifa hiyo, alipewa maelezo na kutahadharishwa kutopokea maelekezo kutoka kwa watu asiowajua.

PSSSF inawasisitiza wastaafu na wanachama wote kuwasiliana na Mfuko pindi wanapohitaji stahiki zao kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ambayo ni kupitia Ofisi zilizopo nchi nzima, Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa Njia ya Simu, Tovuti, na mitandao ya kijamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments