Wednesday, May 20, 2026
spot_img
HomeMichezoSimba yatamba kuchukua pointi  tatu kwa Coastal Union 

Simba yatamba kuchukua pointi  tatu kwa Coastal Union 

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC na Coastal Union utakaochezwa kwenye CCM Mkwakwani Stadium, wekundu hao wa Msimbazi wameonyesha kujiamini wakiahidi kuondoka na ushindi muhimu.

Simba waliwasili jijini Tanga jana na kufanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Mkwakwani mbele ya mamia ya mashabiki waliojitokeza kuwapa hamasa kuelekea mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema kikosi chake kiko tayari kwa pambano hilo licha ya kuikubali Coastal Union kuwa timu yenye ushindani mkubwa.

“Tunawaheshimu Coastal Union, lakini sisi tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu. Wachezaji wangu wako tayari kwa mapambano,” amesema Barker.

Amesema mchezo huo ni muhimu katika mbio za ubingwa, hivyo kila mchezaji anatambua wajibu wake ndani ya uwanja ili kuhakikisha timu inapata matokeo chanya.

Kwa upande wake, kiungo mshambuliaji wa Simba, David Kameta, amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja yuko tayari kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana.

“Tunafahamu Coastal Union wamejiandaa vizuri, lakini nasi tupo tayari kuhakikisha tunashinda,” amesema Kameta.

Ameongeza kuwa Simba imejikita katika kushinda michezo yake yote iliyosalia bila kuangalia matokeo ya timu nyingine kwenye mbio za ubingwa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments