Friday, May 15, 2026
spot_img
HomeAfyaSerikali yaomba Sekta Binafsi kuunga mkono huduma za afya

Serikali yaomba Sekta Binafsi kuunga mkono huduma za afya

Serikali imeziomba taasisi binafsi zinazojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa huduma pamoja na vifaa vya afya kujitokeza kusaidia vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza changamoto zilizopo na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

Wito huo umetolewa leo Mei 15, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati akipokea msaada wa taulo za kike na za watoto 8,000 zilizotolewa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana kwa ajili ya wanawake na watoto.

Msaada huo unatarajiwa kugawiwa bure kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wanawake na watoto wanaohudumiwa katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana, Bryson Kiwelu, amesema vituo vya kutolea huduma za afya vina mahitaji mengi na serikali peke yake haiwezi kuyamudu yote, hasa kutokana na ongezeko la huduma zinazotolewa kila siku.

Amesema ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na serikali katika kusaidia jamii, hususan wanawake na watoto wanaohitaji huduma za msingi za afya.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni ya Daycare amesema msaada huo umetolewa kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, ambapo kampuni hiyo imetenga taulo za wanawake na watoto zenye thamani ya Shilingi milioni 30.

Amesema msaada huo utatolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana, Mbagala pamoja na Kituo cha Afya Chanika kwa ajili ya kugawiwa bure kwa wananchi wanaohitaji huduma hizo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments