Thursday, February 26, 2026
spot_img
HomeMichezoMasauni & Seif Cup yaanza kutimua vumbi

Masauni & Seif Cup yaanza kutimua vumbi

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo ikiwa pamoja na ujenzi wa viwanja na kuangalia fursa mbalimbali ili kuendeleza vipaji kwa vijana.

Ameyasema hayo wakati akizindua Mashindano ya Soka ya Masauni & Seif Cup yaliyoanza kutimua vumbi Februari 25, 2026 katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Zanzibar wakati Kundemba FC ikitoka suluhu dhidi ya Vuga FC.

Hussein amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa ukarabati wa Uwanja wa Matumbaku ili michezo mbalimbali iweze kufanyika katika uwanja huo kama ilivyokuwa viwanja vingine.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza viongozi wa Jimbo la Kikwajuni kuifanya ligi hii kuwa ya Wilaya ambapo sasa inahusisha timu kutoka maeneo tofauti ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia vijana.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Jimbo la Kiwajuni limekuwa mnufaika mkubwa wa uwekezaji wa miundombinu ya kimichezo ambaye serikali imeweka hasa katika viwanja.

Amesema Kikwajuni ina historia kubwa katika michezo kwa kutoa wanamichezo wengi ambao kwa sasa wanacheza ligi mbalimbali Tanzania ndio maana ligi hiyo imekuwa ikifanyika mfululizo ndani ya miaka 15.

Masauni ameongeza tayari kuna ujenzi wa Uwanja wa Kisasa ambao utajumuisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa pete, kikapu na soka ambapo hadi Januari mwakani utakuwa umeanza kutumika.

Naye, Mbunge wa Kundi la Vijana Kanda ya Pemba Zainab Abdallah amesema kuna kila sababu ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa uwekezaji katika sekta ya michezo.

Amesema uwekezaji huo umewafanya vijana waone hii ni sehemu ya ajira na Kikwajuni imeendelea kuwa mfano wa kuigwa kutokana na ushirikiano wa viongozi ambao wamewafanya vijana kuwa pamoja kila mwaka nyakati kama hizi.

Jumla ya Timu 20 zinashiriki msimu huu ikiwa pamoja na KISC FC. Ujama, Urus, Misyuu, Aston Villa, Malindi, Mlandege, Mladu, Vila Coast, Muungano, Medson, Black Fighter, Kwahani, Kilimani, Mafunzo, Real Zanzibar, Rio na Galilaya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments