Tuesday, May 5, 2026
spot_img
HomeBiasharaRuto: Ujenzi kiwanda kusafisha mafuta Tanga fursa EAC

Ruto: Ujenzi kiwanda kusafisha mafuta Tanga fursa EAC

Rais wa Kenya, William Ruto, ameeleza sababu za kupendekezwa kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta (refinery) mkoani Tanga badala ya Kenya, akisisitiza kuwa mradi huo ni wa kikanda, si wa nchi moja.

Ruto ameyasema hayo leo, Jumanne Mei 5, 2026 alipolihutubia Bunge la Tanzania, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini.

Amesema wazo hilo limetokana na majadiliano ya viongozi wa Afrika Mashariki, wakilenga kutumia rasilimali kama mafuta, madini na kilimo kukuza uchumi na ajira.

Ameeleza kama angepata nafasi angepeleka mradi huo Kenya, lakini akasisitiza kuwa ujenzi wake ufanywe Tanga ni faida kwa wote.

“Ukijengwa Tanga ni sawa na umejengwa Kenya, kwa sababu sisi ni wamoja,” amesema Ruto.

Aidha, amesema kuwepo kwa bomba la mafuta ghafi Tanga utarahisisha usafirishaji na kupunguza utegemezi wa nishati hiyo kutoka nje ya nchi.

Pia, amesema ukaribu wa Tanga na Mombasa unaongeza faida ya kiuchumi na urahisi wa usambazaji wa mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments