Klabu ya Chelsea FC imemtimua rasmi kocha mkuu Liam Rosenior baada ya kudumu kwa miezi minne kufuatia matokeo yasiyoridhisha ndani ya timu hiyo ya “The Blues.”
Uamuzi huo unakuja baada ya Chelsea kupoteza mechi tano mfululizo, hali iliyoongeza presha kubwa kwa benchi la ufundi pamoja na uongozi wa klabu hiyo ya Premier League.
Kwa sasa, Chelsea imeanza mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayesaidia kurejesha uthabiti na ushindani ndani ya kikosi hicho.




