Mwanamke wa nchini Kenya aliyefahamika kwa jina la Rachel Wandeto, ambaye aliwahi kusambaa mitandaoni baada ya kuchora tattoo ya William Ruto kifuani mwake, ameripotiwa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kufuatia shambulio la kuchomwa moto kwa petroli.
Rachel Wandeto alidaiwa kushambuliwa na watu wasiojulikana katika eneo la Mwiki jijini Nairobi na kuachwa na majeraha makubwa ya moto kabla ya kulazwa hospitalini kwa matibabu.
Kifo chake kimeendelea kuzua mjadala mkubwa nchini Kenya huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kufanywa na mamlaka husika.




