HomeHabariLengo letu ni kujitegemea-Samia

Lengo letu ni kujitegemea-Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema gawio la Sh1.32 trilioni lililotolewa na mashrika na taasisi za umma ni sehemu ya Serikali ya kuongeza mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa kugharamia shughuli za maendeleo.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Juni 30, 2026 alipohutubia katika hafla ya siku ya Gawio, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema gawio ni sehemu ya lengo la kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi katika kugharimia shughuli za maendeleo.

“Tunakwenda polepole tulikotoka ni mbali, lakini tunakwenda polepole bajeti ya mwaka pengo la kujitegemea imebaki kidogo sana.Tukikaza buti, tukifanya kazi kwa bidi bajeti za miaka miwili ijayo tutakuwa tumefanya vizuri,” amesema Dk Samia.

Dk Samia ameeleza kuimarika ndivyo Serikali inayozidi kuongeza uwezo wa kutekeleza vipaumbele vya maendeleo vya wananchi kwa rasilimali za ndani.

“Tunaelekea kujitegemea wanasema ‘haiwezekani hadi pale inapowezekana? sasa inawezekana tumeona hapa.” amesema Dk Samia.

Mkuu huyo wa nchi, amesisitiza kuwa shabaha yake ni kuona suala la kujitegemea linaondoka.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments