HomeBiasharaMradi wa minara 758 waipaisha Tanzania tuzo za WSIS 2026

Mradi wa minara 758 waipaisha Tanzania tuzo za WSIS 2026

Tanzania imepata heshima ya kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya WSIS Prizes 2026 kutokana na mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano ulioongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini na ambayo hayakuwa na huduma ya mawasiliano nchini.

Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki katika hafla iliyofanyika Geneva, Uswisi, ikiwa ni utambuzi wa mafanikio ya serikali katika kuimarisha miundombinu ya mawasiliano. Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Rais Samia tarehe 10 Aprili, 2026.

Mbali na kutwaa tuzo hiyo, Tanzania ilipata uteuzi katika vipengele saba vya Tuzo za WSIS 2026 na kufanikiwa kuibuka na tuzo mbili kwa ujumla, huku pia ikitunukiwa vyeti vya kutambua miradi iliyofanya vizuri.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments