HomeHabariZaidi ya Shilingi trilioni tano zatumika katika huduma na bidhaa migodini

Zaidi ya Shilingi trilioni tano zatumika katika huduma na bidhaa migodini



●-Mkakati wa ‘Local Content’ waacha alama sekta ya madini nchini Tanzania

●-Kiwango hicho cha fedha kubaki mikononi mwa wazawa kupitia zabuni za ndani

●-Serikali yasisitiza kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali.

Zaidi ya Shilingi trilioni 5.5 zimetumika katika ununuzi wa huduma na bidhaa mbalimbali ndani ya migodi nchini Tanzania, hatua inayothibitisha mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Sera ya Ushirikishwaji wa Wazawa (Local Content) katika Sekta ya Madini.

Hayo yameelezwa leo Julai 8, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa wakati akifungua kongamano la Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba. 

Dk.Kiruswa amesema kuwa,fedha hizo ambazo hapo awali zilikuwa zikienda kwa kampuni ya nje ya nchi, sasa zimebaki mikononi mwa wafanyabiashara, makandarasi, na watoa huduma wa Kitanzania.



Amefafanua kuwa, mafanikio hayo yanatokana na usimamizi madhubuti wa Tume ya Madini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni makubwa ya uchimbaji , kuhakikisha kuwa kipaumbele cha kwanza cha zabuni kinatolewa kwa kampuni zilizosajiliwa nchini na zenye umiliki wa wazawa.

 Takwimu  za ununuzi migodini zinaonyesha kuwa kiasi hicho cha fedha kimeelekezwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uhandisi na Ujenzi, Ukandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya migodi na barabara, Nishati na Mafuta, Usambazaji wa nishati ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya kuendesha mitambo.

Ameongeza kuwa sekta nyingine ni Huduma za Jamii, Utoaji wa chakula, ulinzi, usafirishaji wa wafanyakazi, na vifaa vya kinga kazini (PPE).



Dk. Kiruswa ametoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za kifedha, kuendelea kuwajengea uwezo wa kifedha na kiufundi wajasiriamali wazawa ili waweze kushindana katika zabuni kubwa zaidi, hususan za ununuzi wa mitambo mizito na vipuri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) Dk.Venance Mwase amesema, STAMICO inaunga mkono juhudi za Serikali katika ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa kuandaa mradi wa Rafiki Briqutte.

Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kukuza uchumi wa taifa kupitia uongezaji thamani madini pamoja kutoa ajira kwa vijana kupitia mnyororo wa thamani madini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments