Kocha wa Hispania, Luis de la Fuente, aliwapongeza wachezaji wake kama “timu bora duniani” baada ya ushindi wa kushangaza wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.
De la Fuente, ambaye mara kwa mara alisema Hispania ndio timu bora katika mashindano hayo, aliachwa akifurahi huku La Roja ikiizidi Ufaransa na kufikia fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa Jumapili.
Ilikuwa ni kazi nyingine bora ya kiufundi ya kocha huyo wa Hispania, ambaye alisimamia ushindi wa La Roja katika mashindano ya Ulaya mwaka 2024 na sasa ameishinda Ufaransa katika mechi tatu mfululizo za ushindani.
“Tulianza karibu miaka minne iliyopita na tumekuwa waaminifu kwa wazo hilo na limetufikisha hapa,” alisema de la Fuente akiwaambia waandishi wa habari.
“Leo (jana) tumekabiliana na moja ya timu bora duniani, lakini mbele yao walikuwa na timu bora zaidi. Hilo ni tofauti.”
“Wachezaji hawa wanastahili kila kitu – siku baada ya siku wameonesha kujitolea kwao, mshikamano wao, ukarimu wao, vipaji vyao,” aliongeza de la Fuente kuhusu timu yake.
“Wamefanya mambo magumu yaonekane rahisi.”
CHANZO:ESPN




