HomeHabariMbunge wa Mlimba amwaga chozi mbele ya Waziri Ulega

Mbunge wa Mlimba amwaga chozi mbele ya Waziri Ulega

……Ni Dk Kellen Rose Rwakatare akimlalamikia mkandarasi wa barabara ya Ifakara-Mbingu

Mbunge wa Mlimba (CCM), Dk Kellen-Rose Rwakatare jana alilazimika kumwaga machozi mbele ya Waziri wa Ujenzi, Abdalah Ulega, akimlalamikia mkandarasi wa barabara ya Ifakara-Mbingu.

Akizungumza kwa hisia kali huku akiwa amepiga magoti kwenye mkutano huo, Dk Rwakatare alisema barabara hiyo ni mbovu na inawatesa sana wananchi wa jimbo hilo lakini mkandarasi aliyeko hafanyi lolote kuanza ujenzi.

Mbunge huyo alisema mkandarasi anayetengeneza barabara yao ya kipande cha Ifakara Mbingu amekuwa akisua sua kwa muda mrefu.

“Mheshimiwa Waziri leo uko hapa na mkandarasi yuko hapa amepewa bilioni 10 na hafanyi kitu tunaomba ama atengeneze barabara yetu au arejeshe fedha zetu tumechoka kuona barabara haipitiki na mkandarasi hafanyi lolote,” alisema

“Kama anasema atajenga basi asimame hapa mbele yako mheshimiwa Waziri aseme kwa dhati kabisa ataanza kuijenga lini hii barabara maana imekuwa kero kwa wananchi wangu wa Mlimba,” alisema Dk Rwakatare.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nawewe uko hapa naona hawa watu wanatuchezea sana wakiendelea hivi tunakuomba sweka ndani, mimi nikakaangwa kila siku na wananchi wangu wa Mlimba, kila kukicha ni maneno yah ii barabara kwa hiyo naomba atuambie ataijenga lini,” alisema Dk Rwakatare

Waziri  wa Ujenzi, Abdalah Ulega yeye aliempongeza Mbunge Dk Kellen- Rose Rwakatare kwa namna ambavyo amekuwa akiwasilisha kero za wananchi wa jimbo hilo kwenye mamlaka ili zipate ufumbuzi.

Alitoa pongezi hizo jana wakati wa ziara yake ya kukagua barabara za Wilaya ya Kilombero ambapo alifika kwenye jimbo la Mlimba na kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo pamoja na Mbunge huyo.

“Kwa namna ya kipekee mimi nanyinyi tumshukuru Mbunge wenu, Dk Kellen Rose Rwakatare maana amekuwa mtumishi mwema wa kupeleka habari za maendeleo, nyingi watu wa Mlimba mna mtu mzuri wa kufanya kazi hiyo, meseji zake ni nyingi sana hapa kwangu za kutaka barabara,” alisema

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments