HomeHabariREA yazindua usambazaji wa majiko banifu Mwanza

REA yazindua usambazaji wa majiko banifu Mwanza

📌 Wananchi kununua majiko banifu kwa shilingi 7,500 tu

‎📌 Serikali yabeba asilimia 85 ya gharama

‎📌Milioni 461 kusambaza majiko hayo kwa Wananchi 9,326

‎Misungwi, Mwanza📍

‎Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); imezindua rasmi mradi mkubwa wa usambazaji wa majiko banifu mkoani Mwanza, wenye thamani ya shilingi milioni 461, kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata nishati safi na salama ya kupikia kwa bei nafuu.

‎Uzinduzi huo umefanyika leo alasili (Tarehe 15 Julai, 2026) katika eneo la soko jipya, wilayani Misungwi na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Johari Samizi ambapo amesema Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya REA na kampuni ya Envotec Services Ltd.

‎Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Johari Samizi amewataka wananchi, hasa akina mama, kuchangamkia fursa hiyo ya kipekee kwani majiko hayo yanapunguza matumizi ya kuni na mkaa, huku yakiwa salama kwa afya zao na utunzaji wa mazingira.

‎Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa viongozi wa REA kuongeza idadi ya majiko hayo kutokana na idadi kubwa ya watu waishio Misungwi, ambayo inakadiriwa kufikia takribani wananchi laki nne na nusu.

‎Naye Mtaalam wa Nishati na Jinsia kutoka REA, Dkt. Joseph Sambali, amebainisha kuwa mkoa wa Mwanza umepata mgao wa majiko 9,326. Alifafanua kuwa mradi huo unatolewa kwa njia ya ruzuku ambapo serikali imebeba asilimia 85 ya gharama zote.

‎”Mwananchi atalipa shilingi 7,500 tu kwa jiko moja, wakati thamani halisi ya jiko hilo ni shilingi 55,499. Kiwango kilichozidi cha shilingi 47,999 kimeshalipwa na Serikali,” alisema Dkt. Sambali na kuongeza kuwa ugawaji huu ni mkakati wa kulinda afya na mazingira nchini.


‎Dkt. Sambali alizitaja wilaya zitakazonufaika na mgao huo mkoani Mwanza kuwa ni pamoja na Misungwi, Nyamagana, Ilemela, Ukerewe, Sengerema, Kwimba na Magu.


‎Kwa upande wake, Mwakilishi wa kampuni ya Envotec Services Ltd, Salama Soud, amewahakikishia wananchi kuwa majiko hayo ni salama na yatawaokoa fedha nyingi kama yakitumika ipasavyo.


‎ Alieleza kuwa majiko hayo yanaruhusu hewa safi ya oksijeni kupita kwa urahisi na yana uwezo wa kutumia kuni na mkaa mbadala.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments