HomeMichezoDk. Kareem afichua kilichozuia collabo na 50 Cent

Dk. Kareem afichua kilichozuia collabo na 50 Cent

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Dk. Kareem, amerejea kwenye tasnia ya muziki kwa kuachia wimbo mpya unaoitwa Depetupu, akisema analenga kupanda chati na kuwa msanii namba moja nchini Tanzania.

Dk. Kareem ameiambia MaarifaOlineMedia kuwa aliwahi kupata matumaini ya kufanya kazi na msanii maarufu wa Marekani, 50 Cent, baada ya kusikia wimbo wake wa Usilambe Asali kwa Ncha ya Kisu. Hata hivyo, amesema mipango hiyo haikufanikiwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Msanii huyo, aliyewahi kutamba na nyimbo zikiwemo Salam Salam, amekuwa nje ya muziki kwa kipindi fulani kutokana na changamoto za kiuchumi.

Sasa amesema kurejea kwake ni fursa ya kuendeleza safari yake ya kimuziki na kuongeza ushindani katika tasnia ya Bongo Fleva.

Kupitia wimbo wake mpya wa Depetupu, Dk. Kareem anatarajia kuendelea kujenga jina lake na kufikia lengo lake la kuwa miongoni mwa wasanii wanaoongoza nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments