HomeHabariIsmaili CIVIC yahamasisha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Ismaili CIVIC yahamasisha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Jumuiya ya Ismailia kupitia umoja wao uitwao ‘Ismaili CIVIC’, wameshirikiana na wadau wengine kufanya usafi wa kina katika ufukwe maarufu wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili.

Usafi huu umefanywa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku Kuu ya Jumuiya ya Ismaili inayofanyika kila mwaka kati ya mwezi wa tisa na wa kumi kote duniani.

Usafi uliofanyika Coco Beach ni sehemu ndogo ya mkakati mkubwa wa Jumuiya ya Ismailia unaoitwa ‘Lengo Moja, Jamii Moja’ (One Purpose, One Community).

Chini ya mkakati huu, viongozi na wanachama wa tawi la Tanzania la ‘Ismaili CIVIC’ walishirikiana na Aga Khan Development Network (AKDN), Aga Khan Foundation (AFK) pamoja na shirika lisilo la kiserikali la Africraft kutekeleza zoezi hilo la usafi wa ufukwe wa Coco Beach.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, Siku Kuu ya  Jumuiya ya Ismailia imetumika kuendeleza na kusimamia mkakati maalum wa jamii hiyo kuboresha maisha, kukuza umoja, na kuimarisha mahusiano na jamii zinazowazunguka, bila kujali imani, jinsia, au asili ya watu.

“Siku Kuu hii inaendelea kuangazia jinsi gani umoja na ushirikiano katika kushughulikia changamoto za jamii inayotuzunguka, pamoja na kuboresha maisha ya watu wote,” alisema Bw. Kamal Khimji, Rais wa Baraza la Kitaifa la Shia Imami Ismaili nchini Tanzania.

Akiunga mkono maoni haya, bwana Alykhan Dhanani, Mkurugenzi wa Kitaifa wa ‘Ismaili CIVIC’ Tanzania,  alisema: “Zaidi ya watu 250,000 wameshiriki katika shughuli mbali mbali za kujitolea kupitia vituo 5,500 vya Ismaili Civic duniani kote.”

Bwana Dhanani alisema kwa kuungana na washirika wa nje wapatao 1,500, zaidi ya miti milioni 4.5 imepandwa na zaidi ya kilo 213,000 za taka zimekusanywa katika jitihada za kuweka mazingira safi kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Akitoa maoni kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Ismaili Tanzania, bwana Nazir Thawer, alisema ushirikiano wa kusafisha mazingira  unaonyesha usahihi wa maono chanya na mapana  yanayofundishwa na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hio duniani ambae ni Mtoto wa Mfalme Rahim Aga Khan V.

Aga Khan V anasimamia maoni kwamba maendeleo endelevu lazima yazingatie utu wa watu, ustawi wao na kuboresha pamoja na kulinda mazingira yao. 

Kwa kumuunga mkono Kiongozi wao Aga Khan V, Jumuiya ya Ismaili inafanya juhudi mbali mbali kuboresha elimu, huduma za afya, ulinzi wa mazingira, miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, uboreshaji wa makazi na kuzingatia maendeleo ya kiuchumi ya jamii zinazowazunguka.

Kati ya washiriki wa kuu kwenye zoezi la usafishaji wa ufukwe wa Coco Beach ni Shirika lisilo la kiserikali la  Africraft.

“Kuboresha maisha yetu na kulinda ulimwengu wetu hakufikiwi kupitia programu kubwa pekee, bali pia kupitia vitendo vidogo vidogo vya kila siku vinavofanywa na mtu mmoja mmoja au na jamii,” alisema bwana Robertho Njovu wa Africraft.

Akimalizia, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashariki ya Jumuiya ya Ismaili, Bw. Hussein Somji alisema katika ofisi zake na misikiti ya Jumuiya hio,  wanapunguza matumizi ya viyoyozi pamoja na kutumia nishati ya jua, pamoja na kuwahimiza wanachama wao kuchukua taadhari kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Ismaili, Nazir Thawer, alisema tukio hilo linaonyesha maono mapana ya kimataifa yanayopendekezwa na Mtukufu Prince Rahim Aga Khan V kwamba, maendeleo endelevu lazima ya zingatie watu, ustawi wao na mazingira yao.

Vile vile, Shirika la Aga Khan Foundation (AKF) lina unga mkono suluhu za maendeleo zinazopendekezwa na wenyeji na jitihada zao kumaliza umaskini, kuimarisha jamii na  kujenga mustakabali endelevu zaidi.

Akichangia maoni, Mwenyekiti wa Bodi ya Vijana ya Aga Khan, Bw. Hanif Bandali, alisema kuwa wao wamepiga marufuku matumizi ya plastiki katika ofisi zao na inachukua hatua za kimkakati kuunga mkono mitazamo ya kimataifa inayolenga kumaliza uzalishajia wa hewa ukaa ifikapo mwaka 2030.

Aliendelea kusema, wanalenga kujenga utamaduni wa uwajibikaji na ushirikiano, ambapo kila mtu anatambua uwezo wake wa kuleta mabadiliko.

“Mustakabali tunaourithi umetokana na maamuzi na matendo ya wale waliotutangulia, na mustakabali tutakaouacha utaamuliwa na yale tunayochagua kufanya leo,” alisema.

“Leo tumekusanyika sio tu kwa ajili ya kusafisha ufukwe… Bali tunafundiaha na kuimiza mchakato wa kubadilisha taka kuwa bidhaa zenye thamani zaidi (up-cycling), taka zilizokusanywa zinabadilishwa ili ziweze kutumika tena,” alihitimisha bwana Dhanani, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Ismaili Tanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments