KLABU ya Simba SC imefungua shauri la madai ya kimkataba dhidi ya Kocha Mkuu mpya wa Yanga SC, Fadlu Davids, katika Mahakama ya Soka ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ikiitaka ilipwe fidia ya dola za Marekani 45,000 (takribani Sh milioni 124) kwa madai ya kuvunja mkataba bila kufuata taratibu.
Kwa mujibu wa shauri hilo, Davids, raia wa Afrika Kusini, anadaiwa kuondoka kambini mwa Simba nchini Botswana Septemba 2025, baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, kwa lengo la kujiunga na klabu ya Raja Casablanca ya Morocco.
Hata hivyo, shauri hilo lilifunguliwa kabla ya Oktoba 15, 2026, wakati Davids akiwa bado hajajiunga na Yanga. Taarifa za hatua hiyo zimeibuka hadharani siku mbili tu baada ya Yanga kumtangaza rasmi kuwa kocha wake mkuu mpya.
Shauri hilo linahusu madai ya ukiukaji wa masharti ya mkataba kati ya Simba na kocha huyo, huku uamuzi wa FIFA kuhusu madai hayo ukisubiriwa.




