Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariACT-Wazalendo kufanya Mkutano Mkuu kuchagua Mgombea urais

ACT-Wazalendo kufanya Mkutano Mkuu kuchagua Mgombea urais

Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama cha ACT-Wazalendo wamekusanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Mkutano huo mkubwa unalenga kumpata mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Tukio hilo ni sehemu ya hatua muhimu za chama hicho katika maandalizi ya uchaguzi, ambapo wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini wanashiriki kujadili na kuamua hatma ya uongozi wa juu wa taifa kupitia ACT-Wazalendo.

Mkutano huo pia unatarajiwa kuwa jukwaa la kujadili ajenda kuu za kisera, kupitisha maazimio ya chama na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments