Wednesday, March 11, 2026
spot_img
HomeHabariDk. Samia atoa suluhu ya maji Mtumbatu, wananchi wamshukuru

Dk. Samia atoa suluhu ya maji Mtumbatu, wananchi wamshukuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesikia kilio cha wananchi wa Kata ya Mtumbatu, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, na kutoa maagizo ya haraka ya kutatuliwa kwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya kampeni alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, ambapo ameeleza kuwa huduma ya maji ni haki ya msingi ambayo kila mwananchi anatakiwa kuipata bila kikwazo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa,Shaka Hamdu Shaka, alifika katika kijiji cha Mtumbatu kuangalia utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia. Alijiridhisha baada ya kuona kazi ya uchimbaji wa vikisima ikiendelea kwa kasi na kumshukuru Rais Samia kwa kusikiliza wananchi wa kata hiyo.

Akizungumza baada ya agizo hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji ya Mto Wami–Ruvu, amesema kuwa kufuatia maelekezo ya Rais yaliyotolewa tarehe 29 Agosti 2025, timu ya wataalamu ilifika Mtumbatu na kufanya tafiti kwenye vitongoji vyote zaidi ya tisa vilivyopo kata hiyo.

“Tayari tumefanya tathmini na tumebaini maeneo matatu yenye vyanzo vya maji vya kutosha na salama kwa matumizi ya binadamu. Hii ni hatua kubwa kuelekea utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais,” alisema Mkurugenzi huyo.

Wananchi wa Mtumbatu wameshukuru kwa hatua hiyo, wakibainisha kuwa changamoto ya maji imekuwa kero kubwa kwa muda mrefu, na sasa wanaamini ahadi hii italeta afueni na kuimarisha ustawi wao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments