Mfanyabiashara Jennifer Jovin (Niffer), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Novemba 07,2025.
Ni wiki moja tangu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lithibitishe kumshikilia mfanyabiashara huyo kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya fujo siku ya kupiga kura.






