Tuesday, March 10, 2026
spot_img
HomeHabariPolisi yakiri kumkamata Werema wa Chadema kwa tuhuma za uchochezi

Polisi yakiri kumkamata Werema wa Chadema kwa tuhuma za uchochezi

Siku moja baada ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuripoti kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kutekwa kwa Charles Werema, Mwenyekiti wa Tawi la Madale, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, taarifa mpya zimebainisha kuwa yuko mikononi mwa Polisi.

Werema alidaiwa kuchukuliwa Novemba 12, 2025, majira ya saa saba mchana katika ofisi yake na watu waliodai kuwa ni askari polisi. Baada ya tukio hilo, familia yake ilianza kumtafuta katika vituo kadhaa vya polisi vikiwemo Mbweni, Mabwepande, Madale na Oysterbay, lakini hakupatikana.

Hata hivyo, Novemba 13, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alithibitisha kuwa Werema amekamatwa na anahojiwa kwa tuhuma za kuhamasisha na kuchochea uvunjifu wa amani. Amesema hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments