Timu ya Dodoma Jiji FC inaongoza kwa kucheza rafu nyingi katika Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka raundi ya sita, ikiwa imecheza madhambi 92 katika mechi zake sita za mwanzo.
Timu hiyo imeshinda mchezo mmoja, sare mbili na kupoteza mitatu, ikikusanya pointi tano.
Timu za Pamba Jiji, JKT Tanzania na Namungo zinashika nafasi ya pili kwa madhambi 86 kila moja. Hadi sasa, jumla ya faulo 1,004 zimechezwa kwenye mechi 39 za ligi, zikitolewa kadi 108—kadi 103 za njano na tano nyekundu.
Namungo inaongoza kwa kadi nyekundu mbili, huku Mashujaa FC, JKT Tanzania na Azam FC zikiwa na moja moja. Uwanja wa KMC Complex umeongoza kwa mabao mengi (14), ukifuatiwa na Jamhuri Dodoma (10) na Benjamin Mkapa (9).




