HomeBiasharaBandari ya Fumba yafungua fursa mpya za uwekezaji

Bandari ya Fumba yafungua fursa mpya za uwekezaji

Zanzibar: Equity Group, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), imeongoza ujumbe wa viongozi na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kutembelea mradi wa Bandari ya Fumba, hatua inayolenga kuhamasisha uwekezaji na kuonyesha fursa za maendeleo ya kiuchumi zilizopo visiwani humo.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwaleta pamoja wawekezaji na taasisi za Serikali ili kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza uwekezaji katika miradi ya kimkakati itakayochochea ukuaji wa uchumi.

Equity Bank, ambayo ni mmoja wa wafadhili wakuu wa mradi wa Bandari ya Fumba, imesema itaendelea kuunga mkono uwekezaji katika miundombinu yenye uwezo wa kuchochea biashara, kuongeza ajira na kuimarisha ushindani wa Zanzibar na Tanzania katika soko la kikanda na kimataifa.

Benki hiyo imeeleza kuwa dhamira yake inaenda zaidi ya utoaji wa huduma za kifedha, kwa kuwezesha ushirikiano kati ya wawekezaji wa ndani na wa kimataifa pamoja na mamlaka za udhibiti ili kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji.

Aidha, juhudi hizo zinaunga mkono utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), kwa lengo la kuimarisha biashara ya kikanda, kuvutia mitaji mipya na kufungua fursa zaidi za maendeleo ya uchumi endelevu nchini Tanzania na barani Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments