HomeBiasharaBangu awataka waendesha ghala kuimarisha uadilifu na huduma

Bangu awataka waendesha ghala kuimarisha uadilifu na huduma

Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, amewataka waendesha maghala kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

Akifungua kikao maalumu cha waendesha maghala kilichofanyika mjini Morogoro,  Bangu amesema waendesha ghala wanapaswa kuendana na wakati kwa kuwa waadilifu, kutoa huduma zenye viwango vya juu na kuhakikisha mfumo wa stakabadhi za ghala unaendelea kuwa na tija kwa wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Waendesha ghala Tanzania, Abdulikarim amesema kikao hicho kimeandaliwa kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji, kujadili changamoto zinazowakabili pamoja na kutafuta suluhisho la kuboresha maslahi ya waendesha ghala kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na uendeshaji wa shughuli zao.

Ameongeza kuwa maazimio na maelekezo yaliyotolewa katika kikao hicho yatawasaidia waendesha ghala kuongeza ufanisi wa kazi zao na kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau wote wa sekta ya kilimo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments