Friday, November 7, 2025
spot_img
HomeHabariMpina arejesha fomu za urais baada ya amri ya Mahakama

Mpina arejesha fomu za urais baada ya amri ya Mahakama

Mgombea urais wa Chama cha ACT – Wazalendo Luhaga Mpina alivyoingia katika Ofsi za Ofsi Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kurudisha fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Mahakama Kuu Dodoma kutoa amri fomu yake ipokelewe.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kutoa amri kwamba Tume hiyo ipokee fomu zake, ikibatilisha uamuzi wa awali uliokuwa umezuia usajili wake katika mchakato huo.

Mpina, ambaye amekuwa akiwania nafasi hiyo kupitia chama chake, amepokelewa na wafuasi na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo muhimu. Wengi wamelitaja tukio hili kama ishara ya ushindi wa kisheria na hatua muhimu kwa demokrasia ya uchaguzi nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments