Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeElimuTanzania yalenga uchumi wa Dola trilioni 1

Tanzania yalenga uchumi wa Dola trilioni 1

Tanzania imeweka malengo ya kufikia uchumi wa Dola trilioni moja kwa kuweka mazingira rafiki ya kuvutia uwekezaji kutoka nje.

Tanzania pia imeweka lengo la kuwa miongoni mwa nchi tatu bora Afrika zenye mazingira rafiki ya kuvutia uwekezaji wa ndani nan je.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa  Viwanda na Biashara, Judith Kapinga  wakati alipokitembelea  Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwaajili ya kujitambulisha katika mwendelezo wa ziara zake katika taasisi zilizo chini ya wizara yake.

Aliagiza miradi yote ya chuo iendelee kutekelezwa kwa weledi na ufanisi mkubwa na kuhakikisha inakamilika ndani ya muda wa mkataba uliosainiwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

“Kwa kuwa miradi hii ni kwaajili ya kuongeza ufanisi basi sisi tunapenda ikamilike kwa haraka ili yale ambayo tunategemea yatatimia baada ya miradi hiyo basi yatimie, nimeona video nzuri ya CBE na nimesikiliza maelezo ya uongozi wa chuo nasisi tunamipango yetu kama Dira ya 2050 tunataka itekelezwe,’ alisema

Waziri alisema kwenye dira ya 2050  serikali imepanga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kati ya uchumi wa viwanda utakaoiwezesha kujitegemea na kufikia dola trilioni moja.

Alisema Tanzania inapanga kuwa miongoni mwa nchi tatu Afrika zinazoongoza kwa kuvutia uwekezaji na kwamba dira ya maendeleo inasisitiza uchumi shindani na bunifu na uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu.

Aidha, alisema hakuna namna ya kufikia malengo yaliyoko kwenye Dira ya taifa kama hakuna vyuo imara vyenye kutoa elimu bora ya biashara na fedha kama chuo cha CBE.

Alisema CBE inatarajiwa kuwa  itakuwa mhimili wa utekelezaji wa vipaumbele vya sekta ya baishara  vilivyomo kwenye  Dira  ya taifa ya 2050 kwa kutoa elimu ya taaluma mbalimbali yenye tija kwa  kwa vijana.

“Naiona CBE kama kiwanda cha maarifa ambacho kinazalisha wataalamu bora wa biashara, masoko,  na teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na kama hatufanyi hivyo naamini tunapaswa kufanya mabadiliko ili tuendelee kuwa kiwanda cha maarifa,” alisema

“CBE inapaswa kuwa kiwanda cha maarifa kwa wizara yetu, chuo kinachotoa tafiti mbalimbali, kwasababu miminaamini nyinyi ndiyo kiwanda cha maarifa cha wizara mtakuwa wachambuzi wa sera wa Wizara kwasababu mna rasilimali za kutosha, tukitaka sera au uchambuzi wa sera tunakuja CBE” alisema Waziri Kapinga

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, alisema CBE imejipambanua kwenye kutoa tafiti zinazolenga kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya viwanda na biashara.

Alisema chuo kimeweka utaratibu wa kutenga rasilimali za ndani kugharamia tafiti mbalimbali zinazofanywa na wahadhiri na watafiti wa chuo hicho .

Alisema katika miaka mitano iliyopita wataalamu wa CBE wamekamilisha tafiti 418 na kuchapisha zaidi ya machapisho 447 katika majarida ya kitaifa na kimataifa.

Profesa Lwoga alisema takwimu hizo zinaonyesha wazi ubora na uzalishaji wa kisayansi wa chuo hicho na mchango wake kwa serikali katika kutatua changamoto za kisera, kiuchumi na kijamii.

“Mfano dhahiri wa mafanikio katika eneo hili ni mkutano wa wa kitaaluma wa mwaka 2025 uliofanyika mkoani Dodoma uliokusanya watafiti, na wanataaluma kutoka ndani nan je ya nchi kuwasilisha matokeo ya tafiti zao kuhusu ustahimilivu wa uchumi na biashara kwa maendeleo jumuishi,” alisema

MwishoT imeweka malengo ya kufikia uchumi wa Dola trilioni moja kwa kuweka mazingira rafiki ya kuvutia uwekezaji kutoka nje.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments