Sunday, March 15, 2026
spot_img
HomeAfyaTunduru Kaskazini wamshukuru Ado kutoa gari la mazishi, wagonjwa

Tunduru Kaskazini wamshukuru Ado kutoa gari la mazishi, wagonjwa

Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ado Shaibu Ado ametekeleza ahadi yake ya kuhakikisha kunakuwepo gari maalum katika Ofisi ya Mbunge kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi na kubebea wagonjwa.

Akitoa ahadi hiyo kwenye Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi uliofanyika katika Viwanja vya Baraza la Idd Mwezi Novemba 2025, Ado alisema ndani ya siku 100 za Ubunge wake atahakikisha kuwa kunakuwepo na gari la kusaidia shughuli za mazishi na kubebea wagonjwa katika Jimbo la Tunduru Kaskazini ikiwa ni sehemu ya kutekeleza wajibu wa kijamii wa Ofisi ya Mbunge.

Ado alisema kuwa ametoa ahadi hiyo kwa sababu anafahamu kuwa wananchi hawana gari la huduma za mazishi na wanalazimika kukodi kwa ajili ya huduma hiyo. Pia alisema licha ya kuwepo kwa magari ya kubebea wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya na Vituo vya Afya vya Tarafa za Nakapanya na Matemanga, bado magari hayo yamezidiwa kutokana na mahitaji makubwa hivyo uwepo wa gari katika Ofisi ya Mbunge utasaidia pale ambapo huduma ya gari la wagonjwa katika eneo husika ina changamoto.

Wakizungumza katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Tunduru jana baada ya kuwasili kwa gari hilo, wanachi wamemshukuru Mbunge wa Tunduru Kaskazini Mheshimiwa Ado kwa kutekeleza ahadi zake na kumtaka kuyatazama maeneo mengine.

Mbali na Kituo cha Wagonjwa, Ado aliahidi pia kuwa ndani ya Siku 100 atahakikisha maboresho jengo la wauguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Kuanzisha Programu ya HAKUNA KUKAA CHINI kwa ajili ya kukusanya rasilimali za kutokomeza tatizo la madawati na kuanzisha mpango maalum wa kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo kwa mikopo isiyo na riba mbali na ile inayotolewa na Halmashauri.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments