Kampuni ya Bolt inaamini kwa dhati kuwa madereva wenye kuridhika hutoa huduma bora Zaidi kwa abiria.
Kwa misingi hiyo, Bolt imejizatiti kuwaheshimu na kuwatendea haki madereva wake,sambamba na dhamira ya kutoza kamisheni ndogo ikilinganishwa na baadhi ya washindani wake sokoni.
Kupitia taarifa hii, Bolt inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu namna offer inavyofanya kazi katika jukwaa lake. Iwapo abiria atapatiwa punguzo la nauli, kwa mfano punguzo la asilimia 40, abiria hulipa kiasi cha fedha kinachooneshwa kwenye programu (app). Sehemu ya fedha iliyopunguzwa, Bolt huilipa moja kwa moja kwa dereva mara baada ya safari kukamilika.
Hatua hiyo ina maana kuwa dereva hulipwa mapato yake yote ya safari husika bila
kupunguzwa, hata ikiwa abiria amepata offer.Madereva ni mhimili mkuu wa huduma za Bolt, na uwezo wao wa kupata kipato cha uhakika ndio msingi wa shughuli zote za kampuni. Kipaumbele cha Bolt ni kuendesha jukwaa lenye haki, uwazi na uhakika, linalolinda na kuendeleza kipato endelevu cha madereva, huku likiendelea kuwapatia abiria uzoefu chanya wa usafiri.





