Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeElimuWanafunzi 725 wapatiwa mafunzo uokozi

Wanafunzi 725 wapatiwa mafunzo uokozi


Jumla ya wanafunzi 725 wa Shule za Butimba A na B wamepata mafunzo ya huduma ya kwanza kwa mtu aliyezama maji, yakitolewa na Chuo cha Polisi Wanamaji Tanzania kama sehemu ya kampeni ya elimu kwa jamii.

Mafunzo hayo yaliongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Kagemula Muhula, aliyesema lengo ni kuwajengea wanafunzi uwezo wa kukabiliana na majanga ya ajali za majini na kutoa msaada wa haraka kabla ya wahudumu wa afya kufika.

Mbali na nadharia, wanafunzi walijifunza kutambua na kutumia vifaa vya uokozi majini wakati wa dharura.

Elimu ni kinga—kutoa maarifa ni kuokoa maisha.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments