Sunday, March 22, 2026
spot_img
HomeAfyaEU yatoa bilioni 1.3 mafunzo kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka

EU yatoa bilioni 1.3 mafunzo kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka

Jumuiya ya Ulaya (EU), imetoa Euro 443,989 kwa taasisi nne nchini kwaajili  ya mradi wa  kutoa mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa sekta ya afya kuhusu namna ya kudhibiti na kutibu magonjwa yanayovuka mipaka duniani.

‎Wanufaika kwenye mradi huo ni Chuo Kikuu Kairuki,  ReadLab, Chuo Kikuu cha St Francis Ifakara na Taasisi ya Mafunzo ya Tanzania Training Center for International Health Ifakara.

‎Akizungumza  kwenye mafunzo ya mradi huo unaotambuliwa kama BRIDGE, Mratibu wa mradi huo kutoka Chuo  cha St Francis Ifakara, Profesa Senga Pemba alisema mradi huo unalenga kusimamia na kuinua elimu ya juu.

Aliwataja wanufaika wengine wa mradi huo kutoka nje ya nchi kuwa ni Chuo Kikuu cha Bologna na Chuo Kikuu cha Athens Ugiriki.

Alisema mradi huo unalenga kutoa elimu inayovuka mipaka kwa wataalamu wa afya ili wawe na ufahamu wa kutambua na kutibu magonjwa ambayo yanavuka mipaka.

‎Alisema magonjwa hayo ni yale ambayo yanapatikana kwa nchi za Afrika ambayo pia yanapatikana kwenye mataifa mbalimbali duniani.

“Katika mradi huu sisi tunalenga vitu vitatu, moja kuangalia je kuna ufahamu wa elimu kuhusu magonjwa yanayovuka mipaka kwa wataalamu wetu, sisi kwa ufahamu wetu  ni kwamba ufahamu uko kidogo sana kwa hiyo tutawatengenezea kozi za kuwaimarisha kuhusu namna ya kutibu magonjwa hayo,”

“Pia katika mradi huu tutajenga vituo vya umahiri ambavyo vitasimamia utoaji wa elimu hiyo ya kutambua magonjwa yanayovuka mipaka, tutaimarisha elimu kwa kushirikina na wenzetu walioko nje ya nchi,” alisema

‎Alitaja vyuo hivyo kuwa ni chuo kikuu cha Colombia, Chuo Kikuu cha Athens Ugiriki na taaisi moja ya Ugiriki ambavyo vitasaidia taasisi za Tanzania zilizo katika mradi huo namna ya kutoa elimu hiyo kwa wataalamu wake.

‎”Tutatengeneza mitaala ya kozi fupifupi zitakazojumuisha watu kutoka nje ya nchi nasisi tutakwenda nje ya nchi kujifunza namna wanavyomudu kutambua na kutibu maradhi yanayovuka mipaka,” alisema

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kairuki, Profesa Yohana Mashalla, alisema mradi huo ni matokeo ya andiko la mradi baina ya chuo cha Kairuki na Chuo cha St Francis Ifakara.

“Sisi taasisi zinazofundisha madaktari na wauguzi, tulikaa tukaona kuna upungufu kwenye masuala ya kudhibiti magonjwa yanayovuka mipaka (global health), tukaona tuwe na mradi wa kufundisha wachache watakaofundisha wengine katika hospitali mbalimbali nchini,” alisema

‎Profesa Mashalla alisema wameangalia zaidi namna ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs ambayo mengine yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi .

‎”Tutatayarisha kozi za kuwafundishia wataalamu wetu wa sekta ya afya na baada ya miaka mitatu mradi utakapoisha tutatafuta mfadhili mwingine wa kufanya mradi huo kuwa endelevu,” alisema

‎Saturini Manangwa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Ubora na Huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya, alisema mradi huo ni muhimu kwani utavijengea uwezo vyuo vya ndani kutambua na kutibu magonjwa yanayovuka mipaka.

‎Alisema watalaamu watatengeneza kozi za kimataifa ambazo zitachangia kuwajengea uwezo watoa huduma wa ndani na kwamba maeneo ya kipaumbele kama kuimarisha utoaji wa huduma.

‎Alisema wataangalia maeneo mengine kama huduma za dharura huduma za upasuaji, na huduma za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo kwa sasa yamekuwa janga kubwa duniani.

‎”Nmatumaini yetu sisi wizara kwamba kwenye mradi huu tutapata matunda mazuri kwa taasisi husika, watoa huduma na wananchi kwa ujumla,” alisema

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments