Monday, March 23, 2026
spot_img
HomeMichezoArsenal City waandika historia Fainali Carabao

Arsenal City waandika historia Fainali Carabao

Timu za Arsenal na Manchester City ziliweka historia katika michuano ya Kombe la Carabao hata kabla ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Timu hizo zilitinga fainali baada ya kuziondoa Chelsea na Newcastle United katika hatua ya nusu fainali. Mara ya mwisho kukutana kwenye mashindano hayo ilikuwa mwaka 2018, ambapo kikosi cha Pep Guardiola kilishinda mabao 3-0.

Fainali hiyo pia iliweka rekodi ya kipekee, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu iliyo nafasi ya kwanza na ya pili katika Ligi Kuu England kukutana kwenye fainali ya Kombe la Ligi.

Kila timu ilipewa tiketi 32,000, huku mechi hiyo ikiwa ya kwanza kufanyika chini ya sheria mpya kali dhidi ya kuingia uwanjani bila tiketi halali. Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa UEFA Euro 2020, ambapo mashabiki wengi waliingia uwanjani bila tiketi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments