Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), David Nchimbi, aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, pamoja na ujumbe wao, waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha, leo tarehe 23 Machi 2026.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Shirika hilo katika kuimarisha mawasiliano Zanzibar kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Ndugu David Nchimbi, amemshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa ushirikiano unaoendelea kati ya Shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.






