Wednesday, April 29, 2026
spot_img
HomeBiasharaBolt Tanzania yatwaa tuzo ya usafiri wa mtandao mjini 2026

Bolt Tanzania yatwaa tuzo ya usafiri wa mtandao mjini 2026


Dar es Salaam, 28 Aprili 2026
 — Kampuni ya Bolt Tanzania imetunukiwa tuzo ya Kampuni Bora ya Usafiri wa Mijini na Ride-Hailing kwa Mwaka katika hafla ya Africa Transportation Excellence Awards 2026 iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo, Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, alisema mafanikio hayo ni ishara ya kasi ya mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya usafiri nchini Tanzania.

“Bolt inafanya kazi katika zaidi ya nchi 50 duniani, na mwaka 2025 Tanzania iliibuka kuwa miongoni mwa masoko yanayokua kwa kasi zaidi barani Afrika, na ya pili duniani baada ya Uswisi. Ukuaji huu unaonesha hitaji la suluhu jumuishi za usafiri zinazotumia teknolojia,” alisema.

Bolt ilikuwa kampuni ya kwanza nchini kuingiza bodaboda na bajaji katika mfumo wa usafiri wa mtandao, hatua iliyopanua huduma kwa mamilioni ya abiria hususan katika jamii za kipato cha kati na cha chini.

Kanyankole aliipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa sekta ya usafiri. Alibainisha kuwa ubunifu endelevu unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sera na sekta binafsi.

Aidha, alitoa shukrani kwa maelfu ya madereva washirika na abiria wanaoendelea kuamini huduma za usafiri wa kidijitali.

Bolt imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza, kubuni na kushirikiana na wadau ili kuimarisha mfumo rasmi na endelevu wa usafiri nchini Tanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments