Tuesday, May 5, 2026
spot_img
HomeHabariRuto amsifu Rais Samia kwa uongozi imara

Ruto amsifu Rais Samia kwa uongozi imara

Rais wa Kenya, Dk. William Ruto, amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi bora na kusimama imara wakati wa vurugu za Oktoba 29,2025.

Aidha, amempongeza kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kikanda kati ya Tanzania na Uganda.

Rais Ruto ametoa pongezi hizo mbele ya Bunge la Tanzania, wakati akilihutubia leo Mei 5, 2026, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini tangu awamu ya pili ya utawala wa Rais Samia.

Rais Ruto pia ameeleza kufurahishwa kwake na namna Rais Samia anavyosimamia maendeleo na kuendeleza mshikamano wa karibu zaidi kati ya nchi jirani.

“Ninapaswa kuupongeza uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huu, hasa kwa kusimama imara,” amesema Rais Ruto.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments