Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kupata huduma za msaada wa kisheria utakazoanza kutolewa kuanzia leo hadi Mei 30 mwaka huu mkoani humo.
Mhita ametoa wito huo jana leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Shinyanga.
Amesema huduma hizo zinatolewa bila malipo kwa wananchi wote kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili.
Utoaji wa huduma za Msaada wa Kisheria utafanyika katika Halmashauri zote sita za mkoa ikuhusisha Kata, Vijiji na Mitaa yote iliyopo.




