HomeBiasharaWabunge wapongeza uwekezaji KLICL

Wabunge wapongeza uwekezaji KLICL


Dodoma, Juni 15, 2026: Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamepongeza uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro (KLICL).

Pongezi hizo zimetolewa na wabunge mbalimbali wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano mahususi kwa PSSSF na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika maeneo ya uwekezaji na huduma.

“Uwekezaji huu katika KLICL ni bora na kiwanda hiki ni kikubwa kuliko chochote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tuhakikishe tunakuwa na bidhaa bora sokoni na kiwanda kiendeshwe kibiashara” ameshauri Mabula Mgangila, Mbunge wa Msalala.

Kiwanda cha KLICL kipo mjini Moshi na kinamilikiwa na PSSSF (86%) na Jeshi la Magereza (14%) na kimeajiri watu 294. Aidha, hadi sasa Serikali imewekeza jumla ya Shilingi bilioni 142.

Kwa upande wake, Mbunge Jackson Kiswaga (Kalenga) alipongeza taasisi za umma, PSSSF kwa uwekezaji mzuri kwenye kiwanda na NSSF kwa kuendesha ‘Skimu ya Hifadhi’ katika viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wake, Mbunge Rashidi Shangazi (Mlalo) pamoja na pongezi alishauri sekta binafsi ikaribishwe katika uendeshaji wa kiwanda ili kuongeza nguvu katika masoko na uzalishaji.

Akifafanua kuhusu hoja mbalimbali za Wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo amesema kiwanda kinatoa elimu ya madhara ya uwekaji chapa mifugo na uchunaji usio bora.

“Mifugo ikiwa na chapa na ikichunwa vibaya thamani ya ngozi hupunguza kipato kwa mfugaji,” amesema Mkurugenzi Mkuu Magambo akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa na kiwanda ili kupata ngozi bora.

Akizungumza kuhusu ushirikiano na sekta binafsi, Magambo alisema kiwanda na PSSSF zipo tayari kufanya kazi na sekta binafsi.

“Tunawakaribisha sekta binafsi waje tushirikiane kuendesha kiwanda hiki, hivyo mwenye mawazo na uwezo wa kushirikiana nasi anakaribishwa wakati wowote,” amesema Magambo.

Awali akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo, Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amesema lengo la kuendesha semina hiyo ni kuwajengea uelewa wabunge kuhusu fursa zilizopo KLICL na faida za ‘Skimu ya Hifadh.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments