HomeMichezoSimba yatoa 'thank you' kwa wachezaji saba

Simba yatoa ‘thank you’ kwa wachezaji saba

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na wachezaji saba kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2026/27.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, klabu hiyo imewashukuru wachezaji hao kwa mchango wao ndani ya timu na kuwatakia kila la heri katika hatua zao zinazofuata za maisha ya soka.

Wachezaji walioachwa na Simba SC ni:
👋 Chamou Karaboue
👋 Naby Camara
👋 Edwin Balua
👋 Joshua Mutale
👋 Awesu Awesu
👋 Omari Omari
👋 Moussa Camara

Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya kikosi yanayofanywa na Simba SC kuelekea msimu mpya, huku mashabiki wakisubiri kuona wachezaji watakaojiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments