HomeHabariKatambi: Hatari inaikabili Tanzania, wakoloni wamerudi kwa mbinu mpya

Katambi: Hatari inaikabili Tanzania, wakoloni wamerudi kwa mbinu mpya

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Tanzania inaendelea kukabiliwa na vitisho vinavyofanana na vile vilivyowaleta wakoloni barani Afrika, akieleza kuwa safari hii vinakuja kwa mbinu tofauti.

Katambi ametoa kauli hiyo leo wilayani Karatu, mkoani Arusha, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania, ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

“Taifa letu, kama ilivyo kwingine duniani, linawindwa. Linawindwa si kwa bahati mbaya, ni kwa sababu zilezile zilizowaleta wakoloni hapa, ndizo hizo hizo zinawarudisha kwa namna nyingine,” amesema Katambi.

Amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na umoja, uzalendo na mshikamano ili kulinda maslahi ya taifa dhidi ya changamoto na ushawishi unaoweza kuhatarisha maendeleo na usalama wa nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments