HomeMichezoImbeju–Ndondo Cup yaendelea kuibua vipaji vya vijana

Imbeju–Ndondo Cup yaendelea kuibua vipaji vya vijana

DAR ES SALAAM: Mashindano ya Imbeju–Ndondo Cup yameingia rasmi hatua ya 32 bora kwa mchezo uliowakutanisha Madenge FC na Mzimuni FC kwenye Uwanja wa KMC, huku Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa, akiwa mgeni rasmi.

‎Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hatua hiyo, Tully alisema mashindano hayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwaibua, kuwaunganisha na kuwawezesha vijana kutumia vipaji vyao kama nyenzo ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

‎ “Kupitia Imbeju–Ndondo Cup, tunataka kila kijana aamini kuwa kipaji alichonacho kinaweza kuwa mwanzo wa safari yake ya mafanikio. Tunawahimiza vijana kuendelea kucheza kwa nidhamu, kujituma na kutumia fursa wanazopata kujijengea maisha bora,” alisema.



‎Alisema CRDB Bank Foundation itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuandaa programu zinazowapa vijana fursa za kukuza vipaji, kujiongezea uwezo na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.

‎ “Mafanikio hayaanzi pale unapopata nafasi kubwa, bali unapoitumia vizuri nafasi uliyonayo. Kupitia Programu ya Imbeju tunaamini katika ndoto za vijana na tutaendelea kuwaunga mkono ili wazitimize,” alisisitiza.

‎Hatua ya 32 bora inatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku timu zikisaka nafasi ya kutinga hatua inayofuata ya mashindano hayo, ambayo yameendelea kuvutia mamia ya vijana na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine.



‎Kupitia mashindano hayo, CRDB Bank Foundation, kupitia Programu ya Imbeju, inaendelea kutumia michezo kama chombo cha kuibua vipaji, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuwapa vijana fursa ya kujenga maisha yenye tija.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments