Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeMichezoNdairagije: Simba imenasa lulu kwa kumsajili Bajaber

Ndairagije: Simba imenasa lulu kwa kumsajili Bajaber

Kocha Etienne Ndairagije wa Polisi Kenya amesema Simba imepata mchezaji wa thamani kwa kumsajili Mohammed Bajaber, akieleza kuwa ana kipaji kikubwa cha kutengeneza nafasi na kufunga.

Simba inadaiwa imempa mkataba wa miaka miwili winga huyo wa kimataifa kutoka Kenya.

Bajaber amejiunga na Simba na kuondoka kwenye kikosi cha taifa cha Kenya kinachojiandaa na CHAN, huku Simba ikiwa kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments