Rais wa FIFA Gianni Infantino na Rais wa CAF Patrice Motsepe wamempongeza Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena kuongoza TFF.

Infantino amemtakia Karia na Kamati ya Utendaji mafanikio katika kipindi cha miaka minne ijayo, huku akimshukuru kwa mchango wake katika maendeleo ya soka la Tanzania.
Motsepe naye ameahidi CAF kuendelea kushirikiana na uongozi huo, akisisitiza kuchaguliwa kwake ni ishara ya imani ya wanachama wa TFF kwa uongozi bora.
Viongozi waliyochaguliwa pamoja na Karia ni Athumani Nyamlani (Makamu wa Kwanza wa Rais), Nassor Idrissa (Makamu wa Pili wa Rais), na wajumbe 12 akiwemo Khalid Mohamed, Issa Bukuku, Mohamed Aden, James Mhagama, Somoe Ng’itu na wengine.




