Klabu ya Pamba Jiji imeondoka Mwanza kuelekea Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaoanza Septemba 16.

Timu hiyo chini ya kocha mpya Francis Baraza imekamilisha usajili wa wachezaji wapya akiwemo Abdallah Idd Pina (mfungaji bora Ligi Kuu Zanzibar), Kelvin Nashon (Singida Black Stars), Amos Kadiliko (Fountain Gate), na kiungo wa zamani wa Simba Abdallah Hamisi kutoka Hadiya Hossana (Ethiopia). Wengine ni Hassan Kibailo (Namungo), kipa Arijifu Amour (Azam), na kiungo Siwa Oyugi (Kagera Sugar).
Pamba Jiji inajiandaa Morogoro sambamba na Fountain Gate, huku timu nyingine za Ligi Kuu zikisambaa mikoani kwa kambi; JKT Tanzania na Azam (Arusha), KMC (Zanzibar), Mtibwa Sugar (Dar es Salaam), na Simba SC pekee imekwenda nje ya nchi (Misri) kwa pre-season.




