Wednesday, March 11, 2026
spot_img
HomeMichezoAucho, Singida bado kitendawili

Aucho, Singida bado kitendawili

Hatima ya kiungo wa zamani wa Yanga, Khalid Aucho, kujiunga na Singida Black Stars bado haijakaa sawa licha ya awali kusemekana amesaini mkataba wa miaka miwili.

Habari zinasema klabu hiyo tayari imesajili mchezaji mwingine kuziba nafasi yake baada ya kuonekana “anajivuta” kusaini mkataba na kuchelewa kurudi kambini.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Massanza, amethibitisha tukio hilo, akisema:

“Kocha wetu mpya, Miguel Gamondi, alimpendekeza kama chaguo la kwanza. Tulikubaliana naye, akakubali ofa, lakini akawa anachelewa kuirudisha na kuchelewa kambini, hivyo tukasajili mchezaji mwingine.”

Singida Black Stars ipo kambini Arusha ikicheza mechi za kirafiki kwa maandalizi ya msimu mpya. Hadi sasa wameshasajili wachezaji tisa wapya, akiwemo watano wa kigeni na watatu wa Kitanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments