Dodoma Jiji imemtambulisha kipa Castor Mhagama kutoka KenGold, akiahidi kusimama imara langoni kwa ajili ya malengo ya timu.

Usajili wa kipa huyo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao chini ya kocha mpya Mashami Vicent.
Mhagama anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa baada ya Miraji Ahumani, Edgar William na Faraji Kayanda.




