Chama cha Vishale Tanzania (TADA) kimetangaza kuwa mashindano ya Taifa yatafanyika Agosti 29–31 jijini Dodoma kwa lengo la kupata bingwa na kuunda kikosi cha taifa.

Katibu Mkuu, Joseph Innocent, amesema mashindano hayo yatashirikisha mabingwa wa mikoa na klabu bingwa huku ada ya ushiriki ikiwa Sh 60,000 kwa mikoa na Sh 20,000 kwa klabu.
Washindi watazawadiwa fedha na vikombe.




