“Hivyo katika kipindi hiki rai yangu hususan kwa viongozi wenzangu wa kisiasa ni kudumisha amani kwa kuepuka migongano isiyo ya lazima. Na nayasema haya kwa sababu najua mkutano wetu huu, huko unaangaliwa na wengi nje ya ukumbi huu, kwa hiyo naongea na wote. Amani si kutokuwepo migongano au migogoro, lakini ni kutumia njia za amani kuondosha hiyo migogoro yenyewe, ndiyo kunakoleta amani,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.





