Saturday, March 7, 2026
spot_img
HomeHabariRais Dkt Samia wa kwanza kurudisha fomu INEC

Rais Dkt Samia wa kwanza kurudisha fomu INEC

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Agosti 27, 2025, amewatangulia wagombea wengine wa urais kwa kurejesha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Ndejengwa, jijini Dodoma.

Kitendo hicho kinampa nafasi ya kusubiri uamuzi wa uteuzi kutoka INEC, kabla ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu zitakazodumu kwa siku 60.

Dk. Samia, ambaye ni mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua kampeni za chama chake kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo wa CCM aliwasili katika ofisi za INEC saa 1:50 asubuhi, akiwa wa kwanza kurejesha fomu kabla ya wagombea wengine, kama ilivyokuwa wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk. Samia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho pamoja na mgombea mwenza wake, Dk. Emmanuel Nchimbi. Miongoni mwa waliokuwa naye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira; Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda; pamoja na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments