Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariMoza: Nichagueni nikapiganie Katiba Mpya

Moza: Nichagueni nikapiganie Katiba Mpya

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Chaumma, Moza Ally  amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua ili akapiganie upatikanaji wa Katiba mpya bungeni.

Amesema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Kinondoni, zikiwa zimebaki siku mbili kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

“Nichagueni niende bungeni niende nikapiganie upatikanaji wa Katiba mpya. Nitakwenda kubanana na Waziri wa Katiba hadi kieleweke. Na wakinifukuza mjiandae kunipokea na nitazunguka nchi nzima kuipigania, alisema Moza.

Moza alisema mbali na kupigania upatikanaji wa Katiba mpya pia atahakikisha wananchi wa Kinondoni wanapata majisafi na salama pamoja na mikopo ya asilimia 10.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments